ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 28, 2016

SHINDANO LA MAMA SHUJAA WA CHAKULA LINALOENDESHWA NA OXFAM LAZINDULIWA RASMI MONDULI MKOANI ARUSHA MSHINDI KUONDOKA NA TSH 25,000,000/=

Hatimaye Shindano la Mama Shujaa wa Chakula linaloendeshwa na Shirika la Kimataifa la Oxfam Tanzania limezinduliwa Rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Monduli Idd Hassan Kamanta aliyemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Mrisho Gambo na kuoneshwa  na ITV kila siku (kuanzia 27/09/2016 - 17/10/2016) saa 12.30 jioni, Uzinduzi huo ulifanyika katika kijiji cha Enguiki, wilaya ya Monduli mkoani Arusha na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo mwakilishi wa DED, DAS, wazee wa kimila, wenyeji wa kijiji cha Enguiki, wafanyakazi wa shirika la Oxfam.

 Jumla ya washiriki 15 kutoka mikoa 15 Tanzania wapo katika kijiji cha Enguiki ambapo wataishi katika nyumba za wenyeji wao  kwa muda wa siku 21 huku wakifanya shughuli mbalimbali na kujifunza na mwisho mshindi atakayepatikana atajinyakulia zawadi ya vifaa vya Kilimo vyenye Thamani ya Tsh 25,000,000. 

Washiriki wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula ni pamoja na Lucina Sylivester Assey (Shinyanga), Anjela Chogsasi Mswete (Iringa), Mwanaidi Alli Abdalla (Mjini Magharibi), Marta Massesa Nyalama (Kaskazini Unguja), Christina Machumu (Mara), Betty W. Nyange (Morogoro), Mary Ramadhani Mwiru (Kilimanjaro), Maria Alfred Mbuya (Mbeya), Neema Gilbeth Uhagile (Njombe), Mwajibu Hasani Binamu (Mtwara), Eva Hiprisoni Sikaponda (Songwe), Hidaya Saidi Musa (Tanga), Monica Charles Mduwile (Dodoma), Mary Christopher Lyatuu (Arusha), Loyce Daudi Mazengo (Singida)
Wanakikundi cha burudani wakicheza na kuimba nyimbo za asili wakati wa sherehe za ufunguzi wa shindano la Mama Shujaa wa Chakula uliofanyika katika kijiji cha Enguiki.
Mkuu wa wilaya ya Monduli, Idd Hassan Kimanta(kusho

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.