ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, December 5, 2016

MCHENGERWA ACHUKIZWA NA BAADHI YA WATENDAJI WA VIJIJI AMBAO NI MAFISADI NA WALA RUSHWA

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwawahutubia wananchi wa kijiji cha Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani katika mkutano wa adhara wa kujadili changamoto zinazowakabili hususan migogoro ya ardhi.
(PICHA ZOTE NA VICTOR  MASANGU)

NA VICTOR MASANGU, RUFIJI

IMEELEZWA kuwepo kwa sakata la kutokea kwa migogoro ya ardhi kila kukicha katika Wilaya ya Rufiji  Mkoa wa Pwani  kunachangiwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya watendaji wa vijiji kuendekeza masuala ya rushwa ,ufisadi na kuuza maneo kiholela  hali ambayo inasababisha kuchochea  vurugu na mapigano ya mara kwa mara kati ya jamii ya wakulima na wafugaji .

Hayo yamebainishwa na Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kuweza kukagua shughuli mbali mbali  za kimaendeleo pamoja na kuona  changamoto zinazowakabili wananachi wake ili kuweza kuona namna ya kuzitafutia ufumbuzi.

Mchengerwa alisema kwamba katika Jimbo lake la Rufiji kumekuwepo na baadhi ya wenyeviti wa vijiji na watendaji kuwa na tamaa kwa kuamua kuuza hekari moja ya ardhi kwa kiasi cha shilingi elfu tisa hali ambayo amedai hawezi kuwavumilia na atakikisha anashirikiana na viongozi wa serikali kuvunja mikataba yote kwa wawekezaji waliojipatia maeneo  kinyume cha sheria.

Mbunge wa Jimbo la Rufiji Mohamed Mchengerwa akiwawahutubia wananchi wa kijiji cha Chumbi Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani katika mkutano wa adhara wa kujadili changamoto zinazowakabili hususan migogoro ya ardhi.
(PICHA ZOTE NA VICTOR  MASANGU)
“Jamani wananchi wangu kwa hili suala mimi siwezi kukubaliana nalo hata kidogo yani baadhi ya watendaji wa vijiji wanafanya mambo kinyume cha sheria na taratibu kabisa, wanauza ardhi kwa bei ya shilingi elfu tisa, hapa hili nitalivalia njuga na wawezezaji wote walionunua maeneo inabidi tukae nao tena chini kuwekeana mikataba hii sio sahihi hata kidogo,”alisema Mchengerwa.

Aidha Mchengerwa katika hatua nyingine alisema kutokana  na kuwepo na hali ya sintofahamu kwa wananchi wa  kata nzima ya Chumbi  kuhusiana na suala zima la baadhi ya  watendaji wa kijiji hicho kutuhumiwa  kuhusika kujihusisha na uuzaji wa maeneo na kufanya  ubadhilifu wa fedha amewataka kutomkaribisha mwekezaji wa  yoyote mpaka Mkuu wa Mkoa wa Pwani Injia Evarist Ndikilo atapokwenda kusikiliza kilo chao na  kulitatua sakata hilo la ardhi.

Pia Mchengerwa alisema kuwa maeneo mengi  yameuzwa bila ya kuzingatia sheria na taratibu, hivyo katika eneo la kijiji cha Chumbi anatambua kuna migogoro mingi ya ardhi hiyo katika kulitataua suala hilo atahakikisha anashirikiana na viongozi wa ngazi ya Mkoa kwa lengo la kuweza kurudisha ardhi ambayo imechukuliwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji cha Chumbi Salumu Mtimbuko  ambaye pia ni Diwani wa kata ya Chumbi baada ya kutuhumiwa kuhusika katika uuzaji wa ardhi kiholela na ubadhilifu wa fedha na wananchi alisema kwamba kuna baadhi ya wawekezaji wamenunua zaidi ya hekari 2900 wakati yeye bado ajaingia maadarakani.

WANANCHI  wa kijiji cha Chumbi A,B,na C kata ya Chumbi  Wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanakabiiwa na sakata la kuwepo kwa  migogoro mikubwa ya ardhi inayosababishwa na baadhi ya viongozi wa kijiji kujiuzia maeneo kiholela bila ya kuzingatai sheria na taratibu zilizowekwa hali inayopelekea kuwepo kwa uvunjifu wa amani.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.