ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, December 6, 2016

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFANYA ZIARA YA KUSTUKIZA MAENEO WALIYOONDOSHWA WAMACHINGA BADO CHANGAMOTO ZIPO.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akimhoji mmoja kati ya wafanyabiashara walioko ndani ya eneo la makoroboi jijini hapa na hiki ndicho kilichokuwa kikisilika BOFYA PLAY KUSIKILIZA.

LIVE KUTOKA KILOLELI.
Jembe Fm na GSENGO Blog mapema leo asubuhi kupitia Kazi na Ngoma imezuru eneo jipya la biashara la Kiloleli, hili ni eneo la soko la wazi ambalo wafanyabiashara wadogo almaarufu kama wamachinga wamekutwa wakiweka vigingi kwenye vizimba vyao vipya baada ya wamehamishiwa hapa kupisha bomoa bomoa iliyofanyika katikati ya jiji la Mwanza. BOFYA PLAY KUSIKIA CHANGAMOTO ZILIZOPO.


Ni changamoto kubwa sana kwa wadau hawa kuanza safari mpya ya maisha kibiashara.
Akinamama wenye watoto wao mgongoni na vijana wadogo wameonekana eneo hili wakisota kuchimba mashimo ya kusimika nguzo kwaajili ya kujenga upya vibanda vya biashara eneo hili la Kiloleli.




Ulinzi mkali umeimarishwa hapa, wakati huo huo manung'uniko ya baadhi ya wafanyabiashara yakijikita kukosa maeneo ya kufanyia biashara.
Hakuna Fundi, Pichani, "Pale akinamama na akinadada zetu wanapogeuka kuwa mafundi ujenzi"



Kazi mpya kama inachosha hivi.
Sawa wafanyabiashara hawa wameletwa hapa Kiloleli, lakini pia kumbuka kulikuwa na watu hapa, Jeh waliokuwa hapa wamepewa kipaumbele au nao waliandikishwa upya?
Vijana kizazi kipya na harakati za kusaka maisha mapya... kwa mbaaaaaali ulinzi mkali.




Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.