ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, January 18, 2017

KAFULILA AREJEA RASMI CHADEMA AFUNGUKA KILICHOMRUDISHA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA) Freeman Mbowe akimkabidhi kadi Mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini kupitia NCCR Mageuzi  David Kafulila baada ya kurejea ndani ya chama hicho, tukio lililofanyika leo jijini Mwanza.
KAFULILA:-
-"CHADEMA ndiyo nyumbani kwetu"
-"Asifia ndicho chaa kilichomtengeneza hadi watanzania wakamfahamu"
-Pata kufahamu akiwa nje ya CHADEMA kwa kipindi cha miaka 5 aliishi vipi kisiasa

BOFYA PLAY KUSIKILIZA.


Kutoka kushoto ni mbunge wa jimbo la Bunda mjini Ester Bulaya, waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na Profesa Mwesiga Baregu wakiwa ndani ya kikao cha Kamati kuu CHADEMA.
Kutoka meza kuu.


Mkutano.
CHADEMA YAPATA PIGO TENA KATIKA SIASA.
MAHAKAMA ya Mkoa wa Lindi, imemuhukumu kwenda jela miezi nane, Suleiman Mathew ambaye alikuwa mpinzani wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 katika Jimbo la Mtama.

Mathew ambaye ni Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Lindi na kiongozi mwenzake wa kata wamehukumiwa kwenda jela baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mkusanyiko bila ya kibali.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Mkoa wa Lindi, mbele ya Hakimu Mkazi Godfrey Mhina.

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya kusikiliza mashahidi sita wa upande wa mashtaka na kujiridhisha kuwa ushahidi wao umethibitika bila kuacha shaka.

Waliotiwa hatiani na kupewa adhabu hiyo ni Mwenyekiti Chadema mkoani Lindi, Selemani Methew pamoja na Katibu wa Tawi la Kata ya Nyangamala, Ismail Kupilila.

MBOWE ALAANI

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumzia hatua ya Methew kuhukumiwa kwenda jela, alisema huo ni mkakati ulioandaliwa Serikali ya CCM kudhohofisha upinzani na kuwatisha wasifanye siasa.


Hata hivyo, Mbowe aliwagiza viongozi wa chama hicho nchi zima kuandaa orodha ya kesi walizonazo ili kuziwasilisha jumuiya za kimataifa kuonyesha jinsi upinzani unavyo kandamizwa na kupokonywa haki yao ya kufanya siasa.


Alisema Methew amehukumiwa wakati tayari Mbunge wa Kilombero, Peter Lijuakali akiwa ameshahukumiwa kwenda jela miezi sita.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.