ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, February 28, 2017

MWANZA ZIZI NDANI YA JIJI.



 
Na James Timber, Mwanza
MOJA ya barabara za Jijini Mwanza baada ya mvua kunyesha jana. Ilikuwa ni kero kubwa kwa watumiaji wa barabara hiyo inayotoka Soko Kuu. 

Uzoefu unaonesha kwamba mitaro kujaa uchafu husababisha kero hiyo kwani kila mvua inyeshapo jijini hapa lazima maji yatuame na kusababisha daladala kubadili njia na kuleta msongamano wa magari.. 

Bado kuna lawama kwa baadhi ya wanaofanya biashara katika maduka yaliyo kwenye barabara za Jijini Mwanza kwamba wamekuwa wakitupa uchafu katika barabara hizo na kusababisha kuziba mara kwa mara huku lawama nyingine zikiwaendea baadhi ya wanaofanya usafi kwa kufagia uchafu kuelekea kwenye mitaro hiyo. 

Halmashauri ya Jiji la Mwanza inapaswa kuliona hili kama tatizo na kuja na mbinu mbadala ikiwemo faini kali kwa atakayekutwa akitupa ovyo uchafu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.