ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 1, 2017

DC GEITA ANGALIZO: OLE WAKE AMBAYE ATAKAMATWA ANALIMA BANGI.



Mkuu wa Wilaya ya Geita ,Mwl Herman Kapufi akikagua na kuangalia namna ambavyo shamba hilo limelimwa.

Mkuu wa wilaya ya Geita,akiteta jambo na baadhi ya wananchi na mwenyekiti wa mtaa pamoja na diwani wa kata ya Mtakuja kabla ya zoezi la kuondoa zao hilo.

Shughuli ya uondoaji wa Bangi ikiendelea Mkurugenzi wa Mji wa Geita  ambaye amevaa Mkoti wa suti Mhandisi Modest Aporinaly akigoa moja kati ya mmea wa Bangi.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akishughulika.

Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Geita haikuwa nyumba katika shughuli hiyo.

Mwandishi wa Habari wa Storm Fm,na Mmiliki wa mtandao wa Maduka Online Joel Maduka akiendelea na majukumu.

Ulinzi ukiwa umeimalishwa.




Bangi ambayo ilikuwa imekwisha kukomaa kwaajili ya kuuzwa ikioneshwa kwa Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama.

Zoezi la kuchoma likiendelea.

IMEANDALIWA NA MADUKA ONLINE

PICHA NA JOEL MADUKA 
MKUU wa wilaya ya Geita Herman Kapufi ameteketeza na kuvuruga shamba la Bangi  ambalo linasadikika kuwa na ukubwa wa hekari mbili na nusu la Bangi huku akisisitiza kuwa  hakuna mtu yoyote atakeyepona  ndani ya Wilaya yake iwapo atabainika anajihusisha na madawa ya kulevya  ambayo yamekuwa ni hatari kwa vijana wengi.

Mkuu huyo wa Wilaya alitoa kauli hiyo jana wakati wa zoezi la kuteketeza  kwa moto mimea ya bangi kwenye shamba  ambalo lipo  Mtaa wa Samina B kata ya Mtakuja iliyopo halmashauri ya Mji wa Geita.

Kapufi alisema vijana  wengi wanaokaa kwenye vijiwe wanaangamia kwa uvutaji wa bangi na kwamba watu wanaojishughulisha na ulimaji pamoja na usambazaji hatasita kuwachulia hatua kali za kisheria, huku akitoa rai kwa wananchi kuwafichua wanaojihusisha na biashara hiyo haramu.

‘’Ndani ya Wilaya yangu sitasita kuwachulia hatua watu wote wanaojihusisha na ulimaji ikiwemo usambazaji wa madawa ya kulevya  hatuwezi kuona vijana ambao ni nguvu kazi ya taifa wakiteketea kwa madawa hatutakubali…lakini niwashukuru wananchi waliotupatia taarifa kuwepo kwa shamba hili ambalo leo [jana] tunachoma motomimea ya bangi’’alisema Kapufi.

kwa upande wake Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa samina B. John Balenge alisema kuwa walipata taarifa za shamba hilo la bangi kutoka kwa wananchi waliokuwa wakienda porini kufanya shughuli za kutafuta kuni na mkaa na kwamba waliweka mtego wa kumnasa mwenye shamba bila mafanikio.

‘’Ndugu waandishi kama mnavyoona shamba hili linaonesha mwenye nalo alikuwa akilitunza limesafishwa vizuri niseme tu sisi tulipata taarifa kwa wananchi tukawa tunaweka ulinzi wa kumkamata mmiliki ni mwezi sasa bila mafanikio,’’alisema mwenyekiti huyo.

Naye diwani wa kata ya Mtakuja ambaye pia ni makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa geita Constatine Morand alisema hayuko tayari kumuona mtu akifanya biashara ya madawa ya kulevya katika kata yake na kwamba wanamuunga mkono rais katika vita hiyo.

‘’Nitowe wito kwa wananchi wote wa kata ya Mtakuja siko tayari kuona biashara hii ikiendelea kwenye kata yanngu na kuangamiza watanzania wengi…na sisi huku chini tunamuunga mkono rais wetu Dk. John Magufuli katika vita hii waliyoianzisha,’’alisema morandi.

Akizungumza na MADUKA ONLINE mmoja katti ya vijana ambao walikuwa wakitumia Bangi hapo zamani na kuamua kuachana nazo ,Juma Suleiman alisema madawa hayo ya kulevya hayana faida yoyote na badala yake yanatia hasara kwa vijana na kurudisha maendeleo nyuma.

Kutokana na biashara hii ya bangi  kushamiri katika visiwa vilivyoko mwambao wa ziwa victoria, Mkuu wa Wilaya alisema wakimaliza oparesheni maeneo ya nchi kavu watahamishia nguvu majini kwenda kupambana na wafanyabiashara wa zaohilo  haramu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.