ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 1, 2017

RAIS MAGUFULI ALIVYOSHIRIKI JUMATANO YA MAJIVU LEO.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisali katika Ibada ya Jumatano ya Majivu pamoja na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa, Mke wa Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa na Mke wake Mama Janeth Magufuli katika Kanisa Katoliki Parokia ya  Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa wakiwatakia heri ya Masista katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.



Paroko Msaidizi wa Kanisa la Mtakatifu Petro Father Asis akijiandaa Kumpaka majivu kichwani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika Ibada ya Jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa Katoliki Parokiya ya Mtakatifu Petro lililopo Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Wiliam Mkapa mara baada ya Ibada hiyo ya jumatano ya Majivu iliyofanyika katika Kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.